
Vyuo vingine vimebainika kutoa mitaala isiyosajiliwa na vyuo hivyo na vingine kutokuwa na sifa za kuendesha mafunzo ya ufundi.
Baraza hilo lenye mamlaka ya kusimamia elimu ya ufundi nchini limesema bado linavifanyia uchunguzi vyuo vingi nchini ili kuona kama vina tija ya kuendelea kutoa elimu inayokidhi mahitaji ya soko la ajira kimataifa.
KatibuMtendajiwa Baraza hilo Dokta Primus Nkwera amebainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la mitihani lililojengwa na Baraza hilo kwa kushirikiana na Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa NACTE Mhandisi Steven Mlote amesema Baraza hilo limefungua ofisi kwenye kanda saba nchini ili kuweka huduma jirani na maeneo ya vyuo pamoja na kukagua na kuhakiki viwango vya ubora wa vyuo vya elimu nchini.
Baraza la Elimu ya Ufundi NACTE liliundwa na Serikali kwa sheria namba 9 ya mwaka 1997 inayowapa jukumu la kuvisajiri, kudhibiti na kutoa ithibati kwa taasisi na vyuo ambavyo vinatoa elimu ya ufundi na mafunzo.
Endapo vyuo vikibainika kukiuka sheria, Baraza hilo lina mamlaka ya moja kwa moja ya kuvichukulia hatua.
0 comments:
Post a Comment