Baada ya kuanza vibaya kwa kufungwa
na Namibia kwa mikimbio 102, wenyeji Tanzania wamefanikiwa kuuona mwezi
baada ya kuwafunga Botswana kwa mikimbio (runs) 47) katika michuano ya
Afrika kwa wavulana chini ya miaka 19 ya kriketi kwa ajili ya kufuzu
kucheza kombe la Dunia inayoendelea Dar es Salaam.
Tanzania
walishinda tosi na kuanza mchezo kwa kupata mikimbio 174 (all out)
katika ova 44.4 katika inning (zamu) yao huku Botswana wakishindwa
kufikia mikimbio hiyo na kupata runs 127 ( wachezaji wote
wakitolewa-allout) katika ova 46.5.Kocha wa Tanzania, Khali Rehemtulla amesema licha ya kupoteza mechi ya ufunguzi mwishoni mwa wiki, ana mategemeo ya kuwa mabingwa na kufuzu kucheza kombe la Dunia mwakani huko Dhaka, Bangladesh.
Namibia wameendeleza ushindi kwa kuwafunga Nigeria kwa runs 164 wakati Kenya ilifungwa na Uganda kwa runs 26 katika mchezo mkali uliofanyika klabu ya Gymkhana.
Uganda walifanikiwa kupata runs 95/10 (all out) wakati Kenya walipata runs 69/10 ( all out).
Huo ni ushindi wa pili kwa Uganda, baada ya siku ya ufunguzi kuwafunga Botswana kwa wiketi saba.
Licha ya huzuni ya kufungwa na Uganda Jumapili, Kenya walikuwa na furaha mwishoni mwa wiki kwa kuwafunga Nigeria kwa wiketi saba pia katika mechi ya ufunguzi.
Michuano hiyo inaendelea kwa mechi kadhaa kuchezwa.
0 comments:
Post a Comment