TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Tp Mazembe yasajili watatu wa IvoryCoast

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/50429000/jpg/_50429024_kaluyituka_celebrates_semi_2010.jpgTimu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo imewasajili wachezaji watatu wapya toka kwenye timu ya taifa ya Ivory Coast.
Nyota hao ni Roger Assale, Sylvain Gbohouo na Christian Kouame.
Wachezaji hao wamejiunga na Mazembe wakitokea timu ya Sewe Sports kwa mkataba wa miaka mitano ili kuweza kuisaidia timu kwenye ligi ya mabigwa Afrika.
Mshambuliaji Assale na golikipa Gbohouo walikuwemo kwenye timu ya Ivory Coast iliyotwaa ubigwa wa Afrika huko Guinea ya Ikweta.
Huku kiungo Kouame akishiriki kwenye timu ya taifa katika hatua za awali za kufuzu kwa michuano hiyo.
Rais wa Tp Mazembe Moise Katumbi amewaelezea wachezaji hao "ni wachezaji wazuri tunadhani wataleta mabadiliko makubwa, lengo letu ni kuwapa nafasi wachezaji wa Kiafrika wenye vipaji."
Mabigwa hao wa Afrika kwa mara nne watachuana na Mamelodi Sundowns mwezi ujao katika hatua za awali za michuano ya ligi ya mabigwa Afrika.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)