Serikali ya Ubelgiji imetangaza kuwa itaisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo kwa ajili ya kuandaa ratiba ya uchaguzi ujao nchini humo.
Didier Reynders, Waziri Mkuu wa Ubelgiji na ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya Nje wa nchi hiyo amesema kuwa, nchi yake ipo tayari kuisaidia
Kinshasa kwa ajili ya kuandaa ratiba ya wakati wa kufanyika wa uchaguzi
huo. Akizungumza na vyombo vya habari mjini Kinshasa alipokuwa katika
siku ya mwisho ya safari yake nchini humo, Didier alisema kuwa suala la
usalama wa maeneo ya mashariki mwa Kongo linahitajia kuwekewa ratiba
madhubuti itakayosaidia kuhakikisha uchaguzi ujao unafanyika katika
mazingira salama. Tarehe 12 mwezi huu, tume ya taifa ya uchaguzi nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilisambaza ratiba ya uchaguzi, ratiba
ambayo hata hivyo ilikosolewa na viongozi wa vyama vya upinzani nchini
humo. Kwa mujibu wa viongozi wa vyama hivyo vya upinzani, haitowezekana
kupatikana kiwango cha dola bilioni moja za kugharamia uchaguzi mkuu
kama ilivyopangwa. Didier Reynders, Waziri Mkuu wa Ubelgiji amesema
utengaji wa bajeti inayohitajika kwa ajili ya uchaguzi huo unapasa uanze
haraka iwezekanavyo. Akiashiria mauaji ya watu 260 katika mapigano
yaliyojiri mjini Beni mashariki mwa Kongo, kati ya mwezi Oktoba na
Disemba mwaka jana, Reynders amesema kuwa, ni suala la dharura
kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira salama. Weledi wa mambo
wameitaja safari ya ujumbe huo wa Ubelgiji nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kuwa ni uingiliaji wa mambo ya ndani ya taifa
hilo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment