Kundi la kigaidi la ash-Shabab nchini Somalia, limetekeleza shambulizi
dhidi ya ikulu ya rais wa nchi hiyo na kupelekea mtu mmoja kuuawa. Mbali
na kuthibitisha habari hiyo, afisa usalama wa nchi hiyo Abdur Rahman
Muhammad amesema kuwa makombora manne yaliipata ikulu hiyo ya rais huyo
wa Somalia mapema leo. Kundi la ash-Shabab limetangaza kuhusika na
shambulizi hilo. Taarifa iliyotolewa na kundi hilo imesema kama
ninavyonukuu: “Tumeshambulia ikulu, na baadhi ya makombora yamefanikiwa
kuipata ikulu hiyo.” Mwisho wa kunukuu. Polisi imethibitisha tukio hilo
na kuahidi kuwachukulia hatua kali wahusika. Hivi karibuni kundi la ash
Shabab la Somalia lilisambaza mkanda wa video likitishia kufanya
mashambulizi mengine ya kigaidi katika nchi kadhaa ikiwemo Kenya. Weledi
wa mambo wanasema hatua hiyo kuwa imetokana na hasira za kundi hilo
kufuatia kupoteza maeneo mengi liliyokuwa likiyadhibiti yakiwemo yale ya
kistratijia nchini Somalia. Kwa hivyo shambulizi la mjini Mogadishu
dhidi ya ikulu ya Rais Hassan Sheikh Mohamed, linatoa ujumbe kwamba
kundi hilo bado lingali na uwezo nchini Somalia.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment