TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Jeshi Nigeria: Vita na Boko Haram kumalizika karibuni

Jeshi Nigeria: Vita na Boko Haram kumalizika karibuni Mkuu wa jeshi la Nigeria Luteni Jenerali Kenneth Minimah amesema kuwa vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram vitamalizika hivi karibuni. Mkuu wa jeshi la Nigeria ameyasema hayo leo wakati alipowatembelea wanajeshi wa nchi hiyo katika mji wa Baga kaskazini mwa jimbo la Borno huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Jeshi la Nigeria lilisema tarehe 21 mwezi huu kuwa, limeukomboa mji wa Baga kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Boko Haram ambao waliuteka mji huo tarehe 3 mwezi Januari mwaka huu baada ya siku mbili za mapigano.
Mkuu wa jeshi la Nigeria amesema vita karibu vimekwisha na kwamba jeshi hilo litaikomboa miji ya Dikwa, Bama, Gwoza, Marte na maeneo mengine ya Nigeria siku chache zijazo.  Jeshi la Nigeria limeyasema hayo huku nchi jirani na Nigeria zikifanya juhudi za kurejesha amani huko Nigeria kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo tarehe 28 mwezi ujao.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)