Taarifa iliyotolewa jana na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Zeid Al-Hussein imesema kuwa uamuzi uliochukuliwa na Rais wa Myanmar wa kufuta utambulisho wa raia wasio Mabudha ni ukiukaji wa wazi wa haki za kiraia. Zeid Ra'ad Zeid Al-Hussein amesema maafisa wa serikali ya Myanmar wanakataza hata kutumiwa neno la Rohingya ambalo linaarifisha utambulizho wa Waislamu wa nchi hiyo na kwamba jambo hilo linatia wasiwasi. Taarifa hiyo ya afisa wa Umoja wa Mataifa imesema kuwa Waislamu milioni moja wa Manmar wanaishi katika hali ya kusikitisha na kwamba laki moja na 40 elfu miongoni mwao wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mbinyo mkali wa serikali ya Myanmar.
Katika hatua mpya ya kuwakandamiza Waislamu, Rais wa Myanmar ameamuru kubatilishwa vitambulisho vya Waislamu wote nchini humo na kuwazuia kushiriki katika uchaguzi ujao.
0 comments:
Post a Comment