Uchaguzi wa bunge nchini Misri
uliopangwa kufanyika mwezi ujao wa Machi huenda ukaahirishwa baada ya
kushitadi malalamiko kutoka kwa wanaharakati wa kisiasa na kijamii
wanaopinga sheria za sasa za uchaguzi. Wataalamu wa sheria wanasema
sheria za uchaguzi zinakinzana na katiba ya nchi kwani kipengee cha 37
cha sheria hizo kinamzuia raia wa Misri aliye na uraia pacha kugombea
wadhifa wa ubunge ilihali katiba haijaweka kizuizi hicho. Issam
Islambuli, mwanaharakati wa kutetea haki za raia wa nchini Misri amesema
kuwa, sheria ya uchaguzi imetenga viti 8 kwa Wamisri wanaoishi nje ya
nchi ilihali idadi yao ni takriban milioni 10 na kwa mantiki hiyo viti
hivyo haviendani na idadi hiyo na kwamba pana haja ya sheria hiyo
kufanyiwa maekebisho.
Wamisri waishio nje ya nchi wanatarajiwa kuanza kupiga kura kuwachagua wabunge wao kuanzia Machi 21 mwaka huu.
Huku hayo yakijiri, habari za hivi punde
zinasema kuwa mlipuko mkubwa wa bomu umetokea katika mji mkuu wa Misri,
Cairo na hadi sasa Wizara ya Afya inasema mtu mmoja amethibitishwa
kufariki dunia.
0 comments:
Post a Comment