
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Prof. Makame
Mbarawa amesema kuwa, utovu wa maadili kupitia intaneti katika nchi yake
ni changamoto kubwa kwa serikali ya Dar es Salaam. Akizungumza kwenye
mahojiano maalum na Idhaa hii, Waziri Mbarawa amesema katika kutatua
tatizo hilo, serikali imepitisha sheria ya kukabiliana na uhalifu wa
mitandao ikiwa ni pamoja na kuwabana wanaotumia mtandao kueneza mambo
yanayokinzana na maadili kama vile kupakuwa na kusambaza picha za uchi
na filamu za ngono. Kuhusiana na kutumiwa teknolojia katika kutatua
matatizo ya kisiasa nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla, Prof.
Makame Mbarawa amesema teknolojia ina nafasi ya aina yake katika
kupunguza matatizo yanayojitokeza hususan nyakati za uchaguzi katika
nchi za Kiafrika. Amesema maandalizi ya chaguzi mbalimbali barani Afrika
kuanzia usajili wa wapigakura, upigaji kura, kuhesabiwa kura na
kutangazwa matokeo kunaweza kurahisishwa na kuboreshwa zaidi kupitia
teknolojia za kisasa na hivyo kuepusha ghasia na machafuko
yanayoshuhudiwa katika nchi za Kiafrika baada ya chaguzi hizo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment