
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi nchini Komoro
yanaonyesha kuwa chama cha Juwa chenye misimamo ya Kiislamu na
kinachoongozwa na Rais wa zamani Ahmad Abdullah Sambi, kimeshinda katika
maeneo mbalimbali ya nchi kikifuatiwa na chama cha ‘Maelewano ya
Wakomoro’. Kwa mujibu wa tume hiyo ya uchaguzi, matokeo rasmi
yatatangazwa mwezi Machi mwezi ujao. Ushiriki wa wananchi katika
uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumapili, ulifikia asilimia 73. Aidha
theluthi moja kati ya wabunge 24 waliochaguliwa katika uchaguzi huo,
wanatoka chama cha Juwa. Chama cha Ahmad Abdullah Sambi, rais wa zamani
wa Comoro, kilikuwa madarakani hadi mwaka 2011. Kwa upande mwingine,
chama cha Maelewano kwa ajili ya Wakomoro kilichoshika nafasi ya pili,
ni moja ya waitifaki wakubwa wa chama cha Juwa. Ushindi huo unatajwa
kuwa pigo kwa chama tawala cha UPCD ambapo hakuna mgombea hata mmoja kwa
tiketi ya chama hicho aliyeshinda uchaguzi huo. Uchaguzi huo
ulisimamiwa na waangalizi kutoka nchi zenye kuzungumza lugha ya
Kifaransa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment