Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imewaagiza wazalishaji na
wasambazaji wakubwa wa sukari nchini kuingiza Sukari sokoni na
kuhakikisha inapatikana kwa bei ambayo watanzania wanaweza kuimudu.
Maagizo hayo yametolewa baada ya Serikali kuzuia sukari ya nje kuuzwa hapa nchini hali iliyosababisha kupanda kwa bei ya sukari kati ya shilingi 2500 hadi 3000.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira amesema miezi miwili iliyopita
wazalishaji na wasambazaji wa sukari walisema hawawezi kuwekeza
kutokana na soko la sukari nchini kuharibiwa na sukari inayotoka nje
kitendo kilichoilazimu Serikali kutaka kujua njia zinazoingiza sukari
hiyo.
Amesema baada ya Serikali kuchukua hatua za kuziba mianya ya uingizwaji wa sukari bila kodi na kudhibiti sukari inayopita nchini isibaki isafirishwe kwa kujua kuwa sukari inayozalishwa nchini inatosha, ndipo tatizo la uhaba wa sukari likaibuka na kusababisha bei kupanda, na Serikali ikaona haja ya kukutana na wazalishaji na wasambazaji na kufanya makubaliano
Amesema Sukari iliyopo nchini ni tani elfu 40 na endapo itaingizwa sokoni na kuuzwa bila matatizo yoyote Serikali itawapa vibali wafanyabiashara hao kuagiza tani laki 1 za sukari nje ili kufidia kipindi ambacho viwanda hufungwa kwa ajili ya matengenezo kuanzia mwezi April mpaka mwezi Mei ambapo hufunguliwa na kuendelea kuzalisha kama kawaida.
Maagizo hayo yametolewa baada ya Serikali kuzuia sukari ya nje kuuzwa hapa nchini hali iliyosababisha kupanda kwa bei ya sukari kati ya shilingi 2500 hadi 3000.
Amesema baada ya Serikali kuchukua hatua za kuziba mianya ya uingizwaji wa sukari bila kodi na kudhibiti sukari inayopita nchini isibaki isafirishwe kwa kujua kuwa sukari inayozalishwa nchini inatosha, ndipo tatizo la uhaba wa sukari likaibuka na kusababisha bei kupanda, na Serikali ikaona haja ya kukutana na wazalishaji na wasambazaji na kufanya makubaliano
Amesema Sukari iliyopo nchini ni tani elfu 40 na endapo itaingizwa sokoni na kuuzwa bila matatizo yoyote Serikali itawapa vibali wafanyabiashara hao kuagiza tani laki 1 za sukari nje ili kufidia kipindi ambacho viwanda hufungwa kwa ajili ya matengenezo kuanzia mwezi April mpaka mwezi Mei ambapo hufunguliwa na kuendelea kuzalisha kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment