Ndege za kivita za jeshi la Libya mapema leo zimeshambulia ngome za
waasi katika uwanja wa ndege wa Tripoli na kuna habari kwamba jeshi hilo
linapanga kufanya mashambulizi kama hayo katika uwanja wa ndege mjini
Misrata. Habari zinasema kuwa, mashambulizi hayo ni ulipizaji kisasi kwa
shambulizi lililofanywa na kundi la waasi la Fajr dhidi ya uwanja mdogo
wa ndege wa Zintan. Kamanda wa jeshi la anga la serikali, Saqir
El-jaroshi amesema shambulizi dhidi ya ngome ya waasi katika uwanja wa
Maitiga mjini Tripoli umeharibu silaha nyingi za waasi hao ingawa
hakusema iwapo kumekuwa na maafa au majeruhi. Hujuma za serikali dhidi
ya ngome za waasi wa Fajr nchini Libya zimetekelezwa siku chache baada
ya kuteuliwa jenerali mustaafu, Khalifa Haftar kuwa mkuu wa majeshi ya
nchi hiyo. Haftar amesema kibarua chake ni kuhakikisha waasi hao
wanashindwa na kwamba serikali inayotambuliwa kimataifa inarejea mjini
Tripoli. Kwa sasa serikali hiyo inaendesha shughuli zake katika mji wa
Tobruk ulioko mashariki mwa nchi baada ya waasi wa Fajr kuliteka jiji la
Tripoli na kuunda serikali yao hapo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment