Kamati za usalama katika mabunge mawili ya nchini Kenya zimeidhinisha
uteuzi wa Joseph Boinett kama Inspekta mkuu mpya wa polisi nchini humo.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge la kitaifa inayohusika na masuala ya
usalama, Athman Kamama amesema kamati yake imefanya uchunguzi wa kina na
kuridhia Boinett kuwa Inspekta Mkuu mpya wa Polisi. Naye mwenye kiti wa
kamati kama hiyo katika bunge la Seneti, Yusuf Haji amesema Boinett
anazo sifa zinazohitajika kwa kazi aliyoteuliwa kuifanya. Hapo kesho
wabunge wa mabunge hayo mawili watampigia kura Bw. Boinett na iwapo
watamauidhinisha, jina lake litawasilishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta ili
amteue rasmi. Jina la Boinett lilipendekezwa baada ya kujiuzulu Inspekta
mkuu wa zamani wa polisi, David Kimaiyo mwishoni mwa mwaka jana.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment