Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umetangaza kuwa utaipa Sierra Leone
takriban dola milioni 187 ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa
Ebola pamoja na kufufua uchumi wake. Dola milioni 80 zitatumika
kupambana na Ebola huku fedha zingine zikitumika kuimarisha uchumi.
Ahadi hiyo ya IMF imetolewa huko mjini Geneva, Uswisi kunakofanyika
mkutano wa kimataifa wa kujadili njia na mikakati ya kupambana na
ugonjwa hatari wa Ebola. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika
na masuala ya Ebola, David Nabarro amesema, kibarua kikubwa kilichopo
mbele ya viongozi wa dunia ni kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa
kabisa. Marais wa nchi tatu za magharibi mwa Afrika zilizoathiriwa
pakubwa na ugonjwa huo wanahudhuria mkutano wa Geneva. Takwimu
zinaonyesha kuwa, hadi sasa takriban watu 10,000 wamepoteza maisha
kutokana na ugonjwa wa Ebola wengi wao wakiwa ni kutoka nchi za Guinea,
Sierra Leone na Liberia.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment