Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa mwito wa kusakwa na
kutiwa mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya albino
nchini humo. Rais Jakaya Kikwete amezungumzia hali ya usalama wa nchi,
ikiwemo uvamizi wa vituo vya polisi, uporaji wa silaha ulioambatana na
vifo vya askari na kusema, matukio hayo, baadhi yake yana dalili za
ugaidi. Akizungumzia hali ya usalama nchini humo katika hotuba yake ya
mwishomi mwa mwezi Februari, Rais Kikwete pia amekemea vikali vitendo
vya mauaji dhidi albino na kubainisha kwamba, vitendo hivyo
vinafedhehesha, kudhalilisha taifa na kwamba, katu havivumiliki. Rais
Kikwete amekubali kukutana na viongozi na wanachama wa Chama cha Watu
Wenye Ulemavu wa Ngozi, kwa lengo la kuwasikiliza na kuangalia jinsi ya
kumaliza mauaji ya watu hao, yanayofanywa kwa imani ya ushirikina. Rais
Kikwete amesema: "Nimesikitika na mauaji ya ndugu zetu albino. Ni
vitendo vya kinyama ambavyo havitegemewi kufanywa au kutokea katika
jamii yeyote. Naamini ushirikiano wa karibu kati ya serikali na jamii
utatuwezesha kutokomeza mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na
kuliondolea taifa letu aibu hii".
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment