Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, Muswada wa
Marekebisho ya Sheria mbalimbali likiwemo suala la Mahakama ya Kadhi,
utawasilishwa katika Bunge lijalo ukiwa na maudhui ya kuangalia jinsi ya
kuendesha masuala ya imani ya dini ya Kiislamu. Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Mizengo Pinda amebainisha
kwamba, serikali imeridhia kupelekwa kwake baada ya kuwepo maridhiano
baina ya makundi mawili ya dini za Kikristo na Waislamu juu ya
uendeshwaji wa mahakama hiyo. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kama
ninavyomnukuu: “jambo hilo tunalolipeleka Bungeni tunataka tuweke
utaratibu wa kulitambua, kwa kuwa jambo hili linaloombwa na upande wa
pili ni la kusaidia utekelezaji wa maamuzi yao na sio kuingilia masuala
ya jinai, na ni vyema tuone umuhimu wake”. Waziri Mkuu Pinda ameongeza
kuwa, katika muswada huo wenye maeneo 14, Mahakama ya Kadhi ni sehemu ya
tano katika sheria hiyo na kwamba, mapendekezo yake ni pamoja na
kuangalia sheria ya mwaka 1964 inayotamka suala la Uislamu litazamwe na
lirekebishwe na kuja na mawazo yatakayoweka vipengele vitakavyowezesha
mahakama kuamua mambo yao.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment