TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Malalamiko dhidi ya ukiukwaji wa haki za wafanyakazi wa kigeni Imarati

Malalamiko dhidi ya ukiukwaji wa haki za wafanyakazi wa kigeni Imarati Wafanyakazi wa kigeni wanaoishi Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu au Imarati wamefanya maandamano wakitaka kupewa haki zao za kisheria. Maandamano hayo yanafanyika kutokana na kuendelea kukiukwa haki za wafanyakazi wa kigeni katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kuongezeka malalamiko kuhusu suala hilo.
Maelfu ya wafanyakazi hao wa kigeni walikusanyika jana mjini Dubai wakitaka kukomeshwa mwenendo wa kukanyagwa haki zao, kupandishwa mishahara na kuachiwa huru wafanyakazi wenzao wanaoshikiliwa katika korokoro za Imarati.
Wakati huo huo Jumuiya ya Kimataifa ya Vyama vya Wafanyakazi imeitaka Imarati kutekeleza majukumu yake kuhusu haki za wafanyakazi. Tarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo imesema serikali ya Abu Dhabi inawafunga jela wafanyakazi wa kigeni kwa sababu tu ya kudai uhuru na haki zao na za wafanyakazi wenzao na inaruhusu wafanyakazi wa kigeni watendewe maovu.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaripoti kuwa wafanyakazi wengi wa Asia na Afrika nchini Imarati wananyanyaswa kimwili na kingono na waajiri wao na wanachukuliwa kama watumwa. Miongoni mwa mateso wanayopewa wafanyakazi wa kigeni katika Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ni pamoja na kunyang’anywa pasi za kusafiria, kutolipwa mishahara, kufanyishwa kazi kwa kipindi kirefu, kufungwa, kunyimwa chakula, kubakwa na kunajisiwa na mateso ya kimwili. Hali hiyo ya kinyonyaji inayoshuhudiwa Imarati imekuwa ikiripotiwa pia kwa miaka kadhaa sasa katika nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi hususan Qatar na Saudi Arabia.
Malalamiko mengi yanayotolewa dhidi ya nchi hizo za Kiarabu ni kuhusu kiwango na jinsi mishahara ya wafanyakazi wa kigeni inavyotolewa. Mbali na mishahara duni, wafanyakazi hao pia huwa hawapewi mishahara kila mwezi. Ripoti ya Jumuiya ya Kimataifa ya Vyama vya Wafanyakazi, Shirika la Msamaha Duniani na jumuiya za kutetea haki za wafanyakazi zisizo za serikali inasema kuwa wafanyakazi wa kigeni wanaohudumu katika ujenzi wa viwanja vya michezo vitakavyotumika katika fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022 wanalipwa dola 8 tu kwa siku na senti 75 kwa kazi ya ziada ya saa moja na wengi wao hawapewa fedha hizo kiduchu ila baada ya kupita miezi kadhaa. Wafanyakazi hao wanasema wakubwa wao huwanyang’anya pasi za kusafiria ili wasitoe malalamiko ya aina yoyote, na kitendo hiki ni ukiukaji wa sheria za kimataifa za kazi.
Mishahara duni wanayopewa wafanyakazi wa kigeni na ukiukwaji wa haki zao katika nchi za Kiarabu umekabiliwa na upunzani mkubwa wa jumuiya za kutetea haki za binadamu ambazo zinalaani mwenendo huo na kuuita ‘utumwa mamboleo.’
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)