Naibu Balozi wa Sudan Kusini nchini Kenya James P Morgan amesema kuwa msimamo huo umetokana na kuwa Ethiopia na Sudan zinayadhuru mazungumzo ya amani kwa kile alichokitaja kuwa ni 'ukandamizaji'.
Morgan amesema Ethiopia haipaswi kuwa mwenyeji na Sudan isiwe mpatanishi kwa sababu inawapa mafunzo na silaha waasi. Hii si mara ya kwanza kutolewa takwa la mazungumzo ya Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kufanyika nchini Kenya. Serikali ya Juba imesema inafadhilisha mazungumzo kufanyika Kenya kwa sababu nchi hiyo inaelewa vizuri hali ya mambo Sudan Kusini.
Mgogoro wa Sudan Kusini ulianza baada ya Rais Salva Kiir wa kabila la Dinka kumtuhumu Riek Machar wa kabila la Nuer na aliyewahi kuwa makamu wake, kuwa alihusika na jaribio la kupindua serikali yake Desemba 2013. Mgogoro huo uligeuka na kuwa vita vya ndani baina ya vikosi vya serikali na wafuasi wa Machar ambao aghalabu ni wa kabila la Nuer.
0 comments:
Post a Comment