Amesema katika kipindi cha miezi sita watu 15 nchini
Tanzania, Malawi na Burundi wametekwa na kujeruhiwa na wengine kuuawa
akisema watu watatu kati yao wamekumbwa na visa hivyo wiki iliyopita
pekee. Kamishna Zeid amesema mashambulio hayo mara nyingi hulenga watoto
na matokeo yake Albino wanaishi maisha ya woga ikiwa ni pamoja na
kuhofia kwenda shuleni. Rupert Colville msemaji wa ofisi ya haki za
binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema Kamishna Mkuu anataka mamlaka
kuimarisha ulinzi kwa watu wote wenye ulemavu wa ngozi kwenye maeneo
yote yenye mashambulizi na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wote, na
kuhakikisha kwamba matibabu na huduma kwa wahanga na familia zao
vinapatiwa kipaumbele. Nchini Malawi pekee matukio sita yameripotiwa
wiki kumi za mwanzo wa mwaka huu ilihali nchini Tanzania tukio la hivi
karibini ni la tarehe saba Machi ambapo mtoto wa kiume Baraka Rusambo
alishambuliwa na kukatwa kiganja chake. Nchini Burundi albino 19
wameuawa tangu mwaka 2008 na tukio la karibuni zaidi ni la tarehe 12
Disemba mwaka 2014.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment