Kiongozi huyo amesema uchunguzi unaoendelea kuhusu sakata la ‘kuku’ unapaswa kuharakishwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. Imedaiwa kuwa maafisa waandamizi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na Baraza Kuu la Mitihani (KNEC) walipokea hongo kutoka kwa kampuni moja ya uchapishaji nchini Uingereza ili kuipa kampuni hiyo zabuni ya kuchapisha makaratasi ya uchaguzi na mitihani miaka miwili iliyopita. Waziri mmoja wa serikali ya sasa pia anatuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo ya mamilion ya fedha ambayo inajulikana kama ‘kashfa ya kuku’
“Rais hana nia ya kumlinda mtu yeyote hata kama ni waziri na anachosubiri ni matokeo ya uchunguzi unaoendeshwa na Tume ya Kupambana na Ufisadi” amesema afisa mmoja wa ikulu ya Nairobi ambaye hakutaka jina lake litajwe.
0 comments:
Post a Comment