Leo ni Jumatatu tarehe 11 Jamadil-Awwal mwaka 1436 Hijria, inayosadifiana na tarehe Pili Machi mwaka 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 839 iliyopita, alizaliwa Nasiruddin Tusi,
mwanafalsafa, mtaalamu wa hesabati na nujumu na msomi mkubwa wa Kiislamu
huko katika mji wa Tusi, kaskazini mashariki mwa Iran. Nasiruddin Tusi
aliishi katika kipindi cha Hulagu Khan Mongol na mwanaye na kuasisi
kituo kikubwa na cha kwanza cha sayansi
ya nujumu kilichoitwa huko
Maraghe. Kituo hicho kiliasisiwa mwaka 657 Hijria, huko kaskazini
magharibi mwa Iran. Nasiruddin Tusi ameandika vitabu zaidi ya 80 kwa
lugha za Kiarabu na Kifarsi. Vitabu muhimu zaidi vya msomi huyo ni
pamoja na ‘Asasul-Iqtibaas’, ‘Akhlaaq Naaswiri’, ‘Awswaaful-Ashraaf’ na
‘Sharhul Ishaarat.
Siku kama ya leo miaka 1054 iliyopita alifariki dunia Ali bin Issa Rumani, mtaalamu mkubwa wa elimu ya nahwu na fasihi ya Kiarabu. Bin Issa mbali na kutabahari katika elimu ya fasihi ya Kiarabu, alikuwa pia mtaalamu wa elimu za fiqhi, theolojia, na Qur’an. Miongoni mwa vitabu muhimu vilivyoandikwa na Ali bin Issa Rumani ni kile cha ‘I’jaazul-Qur’an’.
Siku kama ya leo miaka 11 iliyopita, mamia ya watu wasio na hatia waliuawa shahidi na wengine kujeruhiwa katika milipuko mikubwa iliyotokea katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (a.s) huko katika miji mitukufu ya Karbala na Kadhimein nchini Iraq. Katika mwaka huo wananchi Waislamu wa Iraq walifanya marasimu hayo kwa hamasa kubwa baada ya utawala wa Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa nchi hiyo aliyeng'olewa madarakani, kupiga marufuku kwa miaka kadhaa shughuli zote za aina hiyo. Miripuko hiyo ya kigaidi ya Karbala na Khadhimein ilitokea katika muendelezo wa machafuko yaliyoanza Iraq baada ya nchi hiyo kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu na Marekani na Uingereza mwezi Aprili mwaka 2003. Licha ya kwamba wahusika wa shambulizi hilo hawakutambuliwa, lakini wananchi wa Iraq na walimwengu waliinyoshea kidole cha lawama Marekani na waitifaki wake kwa kushindwa kuwadhaminia usalama wananchi wa Iraq baada ya uvamizi wao wa kijeshi nchini humo.
Siku kama ya leo miaka 59 iliyopita, nchi ya Morocco ilijipatia uhuru. Morocco iko kaskazini mwa Afrika katika ukingo wa Bahari ya Mediterrania na Bahari ya Antlantic na inapakana na Algeria na Sahara Magharibi. Morocco ilikombolewa na Waislamu mwishoni mwa karne ya Saba Miladia na silsila kadhaa za kifalme zilitawala nchi hiyo. Mapambano ya wananchi Waislamu wa Morocco dhidi ya wakoloni wa Uhispania na Ufaransa yalipelekea nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1956.
Siku kama ya leo miaka 119 iliyopita sawa na tarehe Pili Machi mwaka 1896 mwanafikizia wa Kifaransa Henri Becquerel alivumbua nururishi au Radioactivity baada ya kufanya utafiti katika mada za urani na vitu vinginevyo. Becquerel alikuwa akichunguza urani ndipo alipogundua nururishi. Utafiti wa mwanafikizia huyo wa Kifaransa ulimfanya atunukiwe tuzo ya Nobel mwaka 1903 na miaka mitano baadae aliaga dunia.
Na siku kama ya leo miaka 490 iliyopita, sawa na tarehe 2 Machi 1525, Budapest mji mkuu wa sasa wa Hungary ulitekwa na majeshi ya utawala wa Othmania. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, mfalme wa dola ya Othmania alimshinda mfalme wa Hungary katika vita vya Mohak na hivyo kupanua wigo wa utawala wake hadi kwenye mipaka ya mji wa Vienna huko Austria.

0 comments:
Post a Comment