Viongozi mbalimbali nchini Tanzania wameendelea kutoa salamu za
rambirambi kwa familia ya mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John
Komba, aliyefariki dunia hapo jana. Rais Jakaya Kikwete amesema taifa
limempoteza kiongozi shupavu na aliyekuwa na moyo wa kuwahudumia
wananchi hususan watu wake wa Mbinga Magharibi. Rais Kikwete amesema
marehemu Komba alikuwa muumini wa utawala wa sheria na uadilifu na
kwamba kifo chake ni pigo kubwa kwa taifa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Spika wa Bunge, Bi. Anna Makinda amesema Bunge limempoteza mwanachama
jasiri aliyesimamia haki na kueleza wazi misimamo yake bila ya woga.
Mbunge huyo alifariki dunia hapo jana punde baada ya kufikishwa
katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada kupata maumivu ghafla
akiwa nyumbani kwake.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment