Mahakama Kuu ya Katiba ya Misri imeasema kuwa baadhi ya sehemu za sheria
ya uchaguzi ya nchi hiyo zinakinzana na katiba ya nchi. Mahakama hiyo
leo imepinga ibara moja katika sheria ya uchaguzi ya Misri ambayo
inazigawa wilaya za uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi ujao wa bunge.
Mahakama Kuu ya Katiba ya Misri hivi sasa inapasa iamue iwapo uchaguzi
wa bunge uliopangwa kufanyika Machi 21 uakhirishwe au la. Mohamed Abdel
Wahhab, mmoja wa mawakili ambaye amepinga sheria ya uchaguzi ya Misri
amesema kuwa, uchaguzi wa bunge utaakhirishwa na kwamba mchakato
unapaswa kuanza tangu mwanzo. Pia Rais wa Misri ameamuru sheria hiyo ya
uchaguzi iandikiwe rasimu katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja
akisema kuwa hatua zote za kisheria zinapasa kuchukuliwa ili kuepuka
kuakhirishwa uchaguzi wa bunge nchini humo. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012,
mahakama hiyohiyo yaani Mahakama Kuu ya Katiba ya Misri ililivunja
bunge ambalo wakati huo lilikuwa linadhibitiwa na harakati ya Ikhwanul
Muslimin ikidai kuwa, bunge hilo halikuchaguliwa kwa mujibu wa katiba.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment