Serikali na makundi sita ya wabeba silaha nchini Mali, yametia saini
makubaliano ya amani yenye lengo la kuhitimisha machafuko kaskazini mwa
nchi hiyo. Makubaliano hayo yametiwa saini leo huko Algiers, mji mkuu wa
Algeria. Inaelezwa kuwa Harakati ya Kitaifa ya Ukombozi wa Azawad
imekataa kutia saini makubaliano hayo. Habari zinasema kwamba, kundi
hilo limetaka muda zaidi kwa ajili ya kufanya mazungumzo na makundi
mengine. Maeneo ya kaskazini mwa Mali yamekuwa yakishuhudia machafuko
tangu kulipojiri mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali kuu ya nchi hiyo
hapo mwaka 2012. Mazungumzo ya amani ya Mali yalianza mwezi Julai mwaka
jana chini ya upatanishi wa Algeria. Jana Jumamosi waungaji mkono wa
harakati za upinzani dhidi ya serikali waliandamana katika kulalamikia
mwenendo mzima wa mazungumzo hayo. Inaelezwa kuwa, makubaliano hayo
yamefikiwa ikiwa ni baada ya duru tano za mazungumzo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment