Wapiganaji 8 wa kundi la kigaidi Al-Shabab wameuawa baada ya
kushambuliwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na vya Umoja wa Afrika
katika jimbo la Bakool kusini magharibi ya Somalia. Akizungumza na
waandishi wa habari, kamanda wa jeshi la Somalia katika eneo hilo
Abdirahman Mohammed amesema oparesheni hiyo ya pamoja iliyodumu kwa saa
10 ilifanyika Ijumaa katika mji wa Celbaar. Mohamed amesema wanajeshi
watatu wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa kwenye mapambano hayo. Hata
hivyo kundi la Al-Shabab limedai kuwa zaidi ya wanajeshi 10 wa serikali
wameuawa na kusisitiza kuwa bado wanaudhibiti mji huo. Wakati huo huo
afisa wa serikali ya Somalia amesema vikosi vya serikali tayari vimerudi
kwenye kambi yao baada ya shambulizi hilo. Vikosi vya Somalia
vikisaidiwa na vya Umoja wa Afrika AMISOM vimepata mafanikio makubwa
katika mwaka mmoja uliopita kwa kunyakua miji mikubwa kutoka kwa
wapiganaji wa Al-Shabab
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment