Waziri huyo amenukuliwa akisema kiongozi wa kundi la kigaidi la Emir ambalo lina uhusiano na lile la Daesh (ISIL) nchini Libya lililohusika na mashambulizi ya mabomu mjini al-Gubba ni raia wa Yemen. Al-Dairi pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa silaha kwa jeshi la Libya akisistiza kuwa tishio la kigaidi sio tu ni kwa Libya bali pia eneo lote la kaskazini mwa Afrika na bara Ulaya. Mipaka ya Libya isiokuwa na doria kali imewezesha wapiganaji kuingia nchini humo wakitokea Nigeria, Mali na Niger.
Huku hayo yakijiri kuna ripoti kuwa Italia inatuma vikosi vya kijeshi nchini Libya kulinda maslahi yake nchini humo. Gazeti la nchini Italia la La Stampa limesema askari wa kikosi maalumu cha Italia wanafanya mazoezi ya kukabiliana na magaidi wa Daesh nchini Libya. Imearifiwa kuwa Italia na wasi wasi mkubwa kuwa magaidi wa Daesh wanaweza kuvuriga bomba la gesi litokalo Libya na kupitia chini ya bahari hadi kusini mwa nchi hiyo ya Ulaya.
0 comments:
Post a Comment