TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Makamu wa rais Sierra Leone ajiweka karantini

Makamu wa rais Sierra Leone ajiweka karantini Makamu wa Rais wa Sierra Leone, Samuel Sam-Sumana, ameamua kujiweka karantini kwa hiari baada ya mmoja wa walinzi wake kuaga dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Sumana anakuwa kiongozi wa kwanza mwandamizi ndani ya serikali ya Sierra Leone kuwekwa karantini kutokana na tishio la Ebola. Kiongozi huyo amesema hali yake ni nzuri na kwamba hatua yake ya kukubali karantini ni ya tahadhari tu. Makamu wa Rais wa Sierra Leone atabakia kwenye karantini kwa siku 21 hadi matokeo ya vipimo vya damu yatakapotolewa. Wafanyakazi wake wako chini ya uangalizi wa madaktari.
Mlinzi wa Sumana, john Koroma alifariki dunia wiki iliyopita baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola.
Maradhi ya Ebola yalikuwa yameanza kupungua nchini Sierra Leone lakini katika siku za hivi karibuni visa vipya vya maambukizi vimekuwa vikiongezeka kwa kasi. Tayari ugonjwa huo hatari umeua zaidi ya watu 10,000 katika nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)