
Wananchi wa Jordan wamefanya maandamano mjini Amman dhidi ya utawala
haramu wa Kizayuni wa Israel. Katika maandamano hayo washiriki wamelaani
mkataba wa gesi baina ya nchi yao na utawala wa Kizayuni na wametaka
kukomeshwa mkataba huo mara moja. Aidha wamesisitiza kwamba Jordan
haipaswi kushirikiana kwa aina yoyote na Israel katika ununuzi wa gesi
kwa kuwa gesi hiyo ni mali halali ya Wapalestina. Wameongeza kuwa, fedha
za mauzo yatokanayo na gesi hiyo zinatumiwa na Tel Aviv katika kuwaua
Wapalestina wasio na hatia wala ulinzi. Aidha waandamanaji wameitaja
Israel kuwa ndiye adui wa Waarabu na Waislamu kwa ujumla. Aidha
waandamanaji hao wameitaka serikali ya Amman kuangalia njia mbadala ya
kudhamini nishati yake kwa kuwa nchi hiyo inamiliki vyanzo vingi vya
utajiri hususan katika sekta ya nishati. Maandamano hayo yalifanyika
jana Ijumaa chini ya ulinzi mkali wa askari wa nchi hiyo. Hii si mara ya
kwanza kwa raia wa Jordan kufanya maandamano kama hayo katika
kulalamikia mahusiano yaliyopo kati ya viongozi wa serikali ya Amman na
Israel na kutaka kukomeshwa ushirikiano wowote na utawala huo
uliotapakaa damu za ndugu zao Wapalestina.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment