
Kadhia ya kutozingatiwa uadilifu kwa wanawake na jamii ya kimataifa kwa
mara nyingine, imeitia wasi wasi Umoja wa Mataifa. Phumzile
Mlambo-Ngcuka, mkuu wa wakala wa masuala ya wanawake, ambao unasimamiwa
na Umoja wa Mataifa amezungumzia suala hilo na kusema, licha ya kupita
miaka 20 tangu kupasishwa sheria ya uadilifu kwa ajili ya wanawake huko
Beijing, nchini China, kwa kuhudhuriwa na wajumbe wa nchi 189, lakini
hadi sasa hakuna nchi iliyotekeleza ipasavyo sheria hiyo. Sanjari na
kuonyesha wasi wasi wake kuhusiana na kukosekana uadilifu wa kijinsia
katika nchi tofauti za dunia, Mlambo-Ngcuka amesema kuwa, wanawake wana
fursa chache zaidi ikilinganishwa na wanaume, katika kupata ajira muhimu
na nafasi za usimamizi katika jamii. Ngcuka ameongeza kuwa, mashinikizo
mbalimbali ya kijamii na unyanya
saji wa familia dhidi ya wanawake, ni
tatizo la dunia na kwamba chanzo cha hali hiyo ni kukosekana usimamizi
bora wa haki za binaadamu na uadilifu kwa wanawake katika jamii hizo.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameyasema hayo ikiwa zimesalia siku mbili
tu kabla ya kufanyika sherehe za ‘Siku ya Wanamke Duniani’ ambazo
zimepangwa kufanyika tarehe nane ya mwezi huu na pia kikao cha wiki
ijayo cha tume inayoshughulikia hali ya wanawake katika nchi tofauti
dunia. Amesema kuwa, njia pekee ya kupunguza uhalifu wa kijinsia na
kukosekana uadilifu wa kijamii dhidi ya wanawake ni kufanywa juhudi za
dhati na viongozi wa dunia kwa ajili ya kukabiliana na vitendo hivyo.
Siku chache zilizopita pia kulifanyika kikao cha taasisi ya Umoja wa
Mataifa inayoshughulikia masuala ya wanawake huko nchini Chile ambapo
kulisisitizwa udharura wa kuhitimishwa ubaguzi dhidi ya wanawake. Katika
ripoti iliyotolewa na kikao hicho chini ya kauli mbiu ya ‘Wito kwa
ajili ya Utekelezaji’ Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na
Michelle Bachelet Rais wa Chile waliutaja mwaka 2015, kuwa mwaka wa
kupambana na ubaguzi kati ya wanawake na wanaume na kufuatilia uadilifu
wa kijinsia duniani, sanjari na kumtaka kila mtu kufanya juhudi kwa
ajili ya kufanikisha lengo hilo. Aidha imepangwa katika vikao vijavyo
vya viongozi wa Umoja wa Mataifa, kujadiliwa ripoti yenye kurasa 150 juu
ya udhaifu uliopo katika utekelezaji wa malengo ya uadilifu wa
kijinsia, kuhusu ripoti iliyotiwa saini mwaka 1995 mjini Beijing nchini
China. Katika kongamano la mjini Beijing, viongozi wa nchi kadhaa za
dunia, walitakiwa kufanya juhudi za kupunguza ubaguzi wa kijinsia dhidi
ya wanawake na pia kuondoa vizingiti vya ukosefu wa usawa sanjari na
kupiga hatua 12 mbele za utekelezaji ikiwemo, afya, elimu, ajira,
ushiriki wa kisiasa na pia haki za binaadamu. Hata hivyo na licha ya
kupita miaka 20 tangu kufanyika kikao hicho, uchunguzi wa maoni
unaonyesha kwamba, asilimia kubwa ya wanawake duniani sanjari na
kuteseka, wanakumbana pia na matatizo mengi ya kimaisha. Taasisi ya
Gallup inayojishughulisha na uchunguzi wa maoni, hivi karibuni
ilitangaza kuwa, zaidi ya wanawake bilioni mbili, wanaishi maisha yenye
matatizo mengi. Uchunguzi huo uliofanywa katika zaidi ya nchi 160 za
dunia, unaonyesha kwamba, ni wanawake milioni 620 pekee ndio wanaoishi
katika mazingira yanayoweza kustahmilika ya kimaisha. Aidha uchunguzi wa
wataalamu wa Umoja wa Mataifa unaonyesha kwamba, kukosekana mfumo wa
sheria, kunatajwa kuwa sababu ya ongezeko la vitendo vya ukosefu wa
uadilifu, ubaguzi, unyanyasaji wa kifamilia, ukandamizaji wa kijinsia,
magendo ya binaadamu kwa kuuzwa wanawake na wasichana, ndoa za lazima za
utotoni, kukithiri wanawake wa mitaani, na aina nyingine ya ukatili
dhidi ya wanawake unaoshuhudiwa katika nchi mbalimbali duniani.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment