Mizengo Pinda amesema kuwa, anawaomba viongozi wa dini nchini Tanzania kuungana na serikali kwa ajili ya kutoa elimu juu ya athari za biashara ya madawa ya kulevya na matumizi yake katika jamii. Ameongeza kuwa, kampeni hiyo inapaswa kuanzia misikitini, makanisani na kwenye mikutano yote inayofanywa na viongozi wa dini na wa serikali.
Aidha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesisitiza kuwa, viongozi wa dini wana jukumu kubwa la kuwalea zaidi vijana ili wasijiingize kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu wao ndiyo kundi kubwa zaidi miongoni mwa waumini.
0 comments:
Post a Comment