
Kufuatia kuongezeka ghasia zitokanazo na ubaguzi wa rangi Marekani,
Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi nchini humo amesema uhusiano
baina ya Wamarekani wenye asili ya Afrika na maafisa wa polisi sasa
umegeuka na kuwa mgogoro wa kitaifa. John Boehner katika mahojiano na
Televisheni ya NBC amesisitiza kuwa maafisa wa usalama wa umma hawapaswi
kujihusisha na vitendo vya utumiaji mabavu. Marekani hivi sasa
imekumbwa na mgogoro wa kitaifa. Hiyo ni kauli ya kiongozi nambari tatu
Marekani baada ya rais na makamu wake. Katika mgogoro huo, mamilioni ya
Wamarekani weusi au wenye asili ya Afrika daima wananyanyaswa na
kufanyiwa ukatili wa maafisa wa usalama na polisi wazungu. Katika
kipindi cha mwaka moja uliopita, kumeshuhudia visa kadhaa vya polisi
wazungu wakiwafyatulia risasi na kuwaua kiholela Wamarekani wenye asili
ya Afrika. Katika vitendo hivyo vya unyama na ukatili, polisi huwalenga
na kuwafyatulia risasi washukiwa ambao aghalabu huwa vijana na
mabarobaro. Katika kitendo cha hivi karibuni cha ukatili huo wa polisi
Freddie Gray, Mmarekani mweusi baada ya kutiwa nguvuni na polisi mzungu
alipigwa na kuadhibiwa vikali ndani ya gari la polisi na kisha
kukimbizwa hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata. Akiwa hospitalini
alifariki dunia. Kufuatia tukio hilo, mji wa Baltimore umeshuhudia
machafuko makali zaidi ya mitaani ambapo wananchi wenye hasira
wamejitekeza kwa moto kulalamikia ubaguzi na ukatili wa polisi ya
Marekani. Machafuko hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi katika miaka ya
hivi karibuni. Ikumbukwe kuwa katika historia ya Marekani kumeshuhudiwa
uasi na maandamano ya Wamarekani weusi wakilalamikia ubaguzi wa rangi
nchini humo. Kilele cha malalamikio hayo kilikuwa katika miongo ya 1950
na 1960 ambapo mashinikizo yalipelekea kuidhinishwa sheria kadhaa
ikiwemo sheria ya kuwapa Wamarekani weusi haki ya kupiga kura. Pamoja na
hayo, hivi sasa baada ya kupita zaidi ya miaka 50 tokea kuibuka
mapambano ya haki za kijamii Marekani, Wamarekani wenye asili ya Afrika
wangali wanakabiliwa na ubaguzi mkubwa na dhulma zisizo na kikomo. Hali
imekuwa mbaya kiasi kwamba hivi sasa maafisa kadhaa wazungu katika
kikosi cha polisi Marekani wamefyatuliwa risasi katika kile kinachotajwa
kuwa ni ulipizaji kisasi. Weledi wa mambo wanasema hali kama hivyo
itaitumbukiza Marekani katika mgogoro mkubwa sana wa kiusalama. Marekani
ni moja za nchi zenye idadi kubwa zaidi ya silaha ndogo ndogo miongoni
mwa raia. Inakadiriwa kuwa katika kila Wamarekani watatu, moja au wawili
kati yao wana silaha. Idadi kubwa ya silaha hizo pia ziko mikononi mwa
Wamarekani wenye asili ya Afrika na wasiokuwa wazungu. Kwa msingi huo
inadokezwa kuwa iwapo maandamano hayatapelekea kumazilika vitendo vya
ubaguzi wa rangi na ukatili wa maafisa wazungu katika vikosi vya
usalama, basi natija itakuwa ni kuanza mapambano ya silaha mitaani.
Jamii ya Marekani hivi sasa katika upande moja inakabiliwa na matatizo
makubwa ya ubaguzi wa rangi na katika upande wa pili inakumbwa na
mgogoro wa kiuchumi na kupungua kiwango cha maisha bora katika jamii na
hayo yote yamepelekea kuongezeka mashinikizo ya kila aina. Ni kwa sababu
hii ndio weledi wa mambo wanasema Marekani sasa iko katika dimbwa kubwa
la mgogoro wa kijamii ambao unaweza kuwa hatua ya kwanza ya mapinduzi
au hata vita vya kitabaka na kirangi. Hatua ya John Boehner, Spika wa
Baraza la Wawakilishi ambaye ni kiongozi nambari tatu nchini Marekani
kutumia ibara ya ‘mgogoro wa kitaifa’ katika kufafanua kuhusu machafuko
ya ubaguzi wa rangi hivi sasa nchini humo ni kengele ya hatari kuhusu
kuibuka umwagikaji damu nchini humo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment