
Watu waliokuwa na silaha wameuwa makumi ya raia, wengi wao wakiwa
wanawake na watoto huko Nigeria katika mfululizo wa mashambulizi dhidi
ya vijiji kadhaa katika jimbo la Plateau. Nanzing Bani kiongozi wa jamii
katika eneo amesema kuwa mauaji hayo yalitokea jana wakati watu
waliokuwa na silaha huku wakiwa wamevalia sera za kijeshi walifanya
ufyatuaji risasi wa kiholela dhidi ya raia huko katika eneo la Kardarko
na katika vijiji jirani jimboni Plateau. Kiongozi huyo wa kieneo amesema
kwamba idadi ya waliouawa inaweza kufikia 100. Watu walioshuhudia na
wenyeji wa eneo hilo wamesema kuwa wavamizi walichoma moto majengo na
nyumba nyingi katika eneo hilo. Mashambulizi hayo ya watu wenye silaha
yamepelekea makumi ya wakazi wa eneo hilo la katika jimbo la Plateau
kuzihama nyumba zao.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment