Amesema sehemu muhimu ya ziara yake nchini Kenya ni
kuanzisha maelewano imara na serikali ya Kenya kuhusu hali ya baadaye ya
wakimbizi wa Somalia walioko nchini humo. Guterres amesisitiza kuwa
kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao kunapaswa kuwa kwa hiari kulingana na
makubaliano ya pande tatu ambazo ni Somalia, Kenya na UNHCR ili
kuhakikisha usalama na hadhi ya wakimbizi hao. Mkuu wa UNHCR amesema
pia wamefanya mawasiliano sawa na hayo na rais wa Somalia na wakuu wa
eneo la Juba Land. Katika mkutano wake na Guterres Mei sita mjini
Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisema, uharaka wa kuwarudisha
wakimbizi umesababishwa na tishio la kiusalama linaloikabili Kenya, na
kuongeza kuwa, anataka mchakato huo ufanyike vizuri bila ya kusababisha
matatizo. Serikali ya Kenya ilitangaza mwezi uliopita uamuzi wa
kurejesha nyumbani wakimbizi wa Somalia kufuatia mauaji ya kigaidi
kwenye chuo cha Garrisa ambapo watu 148 waliuwawa na zaidi ya 70
kujeruhiwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment