Msemaji wa jeshi la Nigeria, Kanali Tukur Gusau, amesema kamanda huyo wa kundi la Boko Haram ambaye jina lake halikutajwa, anahojiwa na vyombo vya dola. Kamanda huyo wa wapiganaji wa Boko Haram alitiwa nguvuni katika eneo la Aulari alipokuwa akijificha.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amesisitiza kuwa kambi kadhaa za Boko Haram pia zimeharibiwa katika operesheni hiyo. Kundi la Boko Haram ambalo limetangaza uungaji mkono wake kwa kundi la kigaidi la Daesh limeua karibu watu elfu 20 na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi huko Nigeria na katika nchi jirani. Kundi hilo limezidisha mashambulizi na ukatili nchini Nigeria tangu Rais Muhammadu Buhari aapishwe kuiongoza nchi hiyo nwezi Mei mwaka huu. Buhari ameapa kuliangamiza kabisa kundi hilo la kitakfiri.
0 comments:
Post a Comment