Manchester United Louis van
Gaal alitoa dau mara mbili la pauni milioni 100 kutaka kumsajili Gareth
Bale, 26, lakini lilikataliwa (Sun), Chelsea wamewaambia Tottenham
kutaja bei ya beki wa kushoto Danny Rose, 25- Chelsea wakiwa tayari
kutoa pauni milioni 15 (Daily Mirror), Lazio wamemwambia wakala wa Mario
Balotelli kuwa wako tayari kumchukua kwa mkopo msimu huu, lakini ikiwa
tu watafuzu kucheza Champions League (Daily Mirror), Liverpool
huenda wakasubiri hadi siku ya mwisho kabla ya kupata dau kwa wachezaji
wake isiyowataka kama Balotelli, Fabio Borini na Jose Enrique (Daily
Telegraph), beki wa PSG Thiago Silva anaamini kuwa Angel Di Maria
kuhamia Ufaransa ni kupiga hatua kwenda mbele (Independent), vipimo vya
afya vya Di Maria vimechelewa kwa sababu alikuwa amechoka baada ya
kusafiri kwa saa 20 akitokea Agrentina kwenda Doha (Daily Mail),
Manchester United watamsajili Pedro kutoka Barcelona kwa pauni milioni
20 katika saa 48 zijazo, na huenda pia wakamchukua beki wa kati wa Real
Madrid, Pepe (Daily Mirror), Southampton wametoa dau la pauni milioni 7
kumtaka beki wa kati wa Celtic Virgil van Dijk, 24 ambaye pia
amehusishwa kwenda Arsenal na Manchester United (Daily Express),
Sunderland wanakaribia kukamilisha uhamisho wa mkopo wa viungo Yaan
M'Villa na Leroy Fer kutoka Rubin Kazan na QPR (Shields Gazette), winga
wa Barcelona Adama Traore, 19 anasafiri kwenda Liverpool wakati
akijiandaa kuijiunga na klabu hiyo ingawa amehusishwa na kwenda Bayern
Munich, Manchester City, Manchester United na Sevilla (Sport), Christian
Benteke amepewa jezi namba 9 ya Liverpool, ambayo iliwahi kuvaliwa na
Ian Rush na Robbie Fowler (Daily Express), Manchester United wamemwambia
kipa Andres Lindegaard kuwa anaweza kuondoka (Daily Mail), Newcastle
United wameongeza kasi yao ya kutaka kumsajili Jesse Lingard wa
Manchester United (ESPN), meneja wa Lyon, Hubert Fournier amemwambia
mshambuliaji Alexandre Lacazette anaweza kuondoka kama hana furaha ya
kuichezea klabu hiyo (L'Equipe), Arsenal nao wamejiunga katika mbio za
kutaka kumsajili Denis Cheryshev wa Real Madrid (AS), Manchester City
wanamnyatia Isco wa Real Madrid (Sport), Juventus wamekataliwa dau lao
na Barcelona la kumtaka Javier Mascherano, ingawa mchezaji mwenyewe
anataka kuhamia Italia (Tuttosport), Manchester City wameambiwa wanaweza
kuanza mazungumzo juu ya Kevin de Bruyne wa Wolfsburg lakini waanzie na
dola milioni 78 (Daily Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Cheers!
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment