Maandamano hayo yalifanyika jana katika mji wa Hudur, makao makuu ya eneo la Bakool huko kusini magharibi mwa Somalia. Naibu gavana wa mkoa wa Bakool, Abdullah Ahmad Noor amewaambia waandishi habari kwamba kuna tetesi kuwa askari wa Kiafrika wa kulinda amani nchini Somalia wamehusika na mauaji ya raia wa Somalia katika mji wa Hudur. Amesisitiza kuwa serikali ya Mogadishu imechukua uamuzi wa kuchunguza madai hayo.
Habari nyingine kutoka Somalia zinasema kuwa jeshi la serikali limewatia nguvuni watu 80 wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi la kitakfiri la al Shabab. Wapiganaji wengine 24 wa kundi hilo wamejisalimisha wenyewe kwa polisi ya Somlai na kuliasi kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment