Duru za habari nchini Kenya zimeripoti
taarifa ya kutekwa nyara kiongozi mmoja wa serikali ya nchi hiyo na
kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab la nchini Somalia. Mukhtar
Maalim Adan, ambaye ni afisa utawala katika mji wa Mandera nchini Kenya,
ametekwa nyara na kundi hilo ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi
ya mara kwa mara nchini humo. Maafisa wa polisi wamesema kuwa, Mukhtar
ametekwa nyara alipokuwa safarini kutoka mjini Mandera kuelekea moja ya
miji ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambapo alivamiwa na wanachama wa
kundi hilo na kisha kuchukuliwa kwa gari lake na kupelekwa
kusikojulikana. Hadi sasa polisi bado haijafanikiwa kunasa gari ya
Mukhtar Adan na ingali inaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika wa
tukio hilo. Hata hivyo polisi ya Kenya ina wasi wasi kwamba huwenda
kiongozi huyo wa serikali akawa amepelekwa Somalia na kundi hilo la
kigaidi. Mji wa Mandera uko katika mpaka wa pamoja wa Kenya na Somalia
ambapo unatajwa kuwa njia mojawapo muhimu inayotumiwa na wanachama wa
ash-Shabab kuingilia nchini Kenya na kutekeleza uhalifu wao. Licha ya
kwamba hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na tukio
hilo la utekaji nyara, lakini kidole cha lawama kimeelekezwa kwa kundi
hilo ambalo wiki kadhaa zilizopita, lilitekeleza hujuma kali dhidi ya
Chuo Kikuu cha mji wa Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya na kuua watu
150 wengi wao wakiwa ni wanafunzi.Al-Shabab wamteka nyara kiongozi wa serikali Kenya

150 wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

0 comments:
Post a Comment