Wanamgambo wa wa Boko Haram, wameshambulia vijiji kadhaa kaskazini
mashariki mwa Nigeria. Duru za habari za kieneo zimearifu kuwa, katika
mashambulizi hayo yaliyotokea kwenye vijiji hivyo vya karibu na mpaka wa
Cameroon, wanamgambo hao wamefanya mauaji ya kutisha kwa kutumia
mashoka na kuchoma moto makazi ya raia. Kundi hilo lenye mafungamano na
kundi la kitakfiri la Daesh, limefanya mashambulizi hayo kama ulipizaji
kisasi kufuatia mashambulizi ya jeshi la Chad dhidi ya ngome za Boko
Haram, mashambulizi ambayo yalipelekea makumi ya wanamgambo wa kundi
hilo kuuawa. Inaelezwa kuwa, zaidi ya vijiji 10 vya jimbo la Borno
vinaendelea kudhibitiwa na kundi hilo huku makumi ya wakazi wake
wakiuawa kwa kukatwa na shoka. Mamia ya wakazi wengine wa vijiji hivyo
wamelazimika kuwa wakimbizi nchini Cameroon. Tayari jeshi la Chad
limejibu hujuma hiyo kwa kushambulia maeneo ya wanachama wa kundi hilo
huko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment