TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Mugabe: Siasa za ardhi Zimbabwe hazikuwa sahihi

Mugabe: Siasa za ardhi Zimbabwe hazikuwa sahihi Kwa mara ya kwanza Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe amekiri makosa yake kuhusiana na suala la ardhi lililozua mjadala mkubwa nchini humo mwaka 2000. Taarifa kutoka Harare, mji mkuu wa nchi hiyo zimemnukuu Rais Mugabe akizungumza kupitia televisheni ya taifa kwamba ardhi walizogawiwa watu weusi raia wa nchi hiyo, ni kubwa sana na kwamba hawawezi kuzisimamia. Mugabe ameongeza kuwa, licha ya raia hao kupatiwa ardhi kubwa, lakini wengi wao wameweza kulima theluthi moja tu ya ardhi hizo. Matamshi hayo ya Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 91 yanatajwa kuwa ya kwanza kutolewa na kiongozi huyo. Kwa miaka 10 sasa Zimbabwe ambayo ilikuwa moja ya wazalishaji wa chakula barani Afrika, imegeuka na kuwa nchi waagizaji chakula kutoka nje. Zaidi ya walowezi 4000 wa Ulaya waliokuwa wamehodhi ardhi kubwa za kilimo nchini humo, walilazimishwa kuondoka na ardhi hizo kupewa wenyeji wa Zimbabwe. Nchi za Ulaya zililalamikia vikali marekebisho hayo ya ardhi huko Zimbabwe ambapo baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaamini Rais Mugabe alitumia suala hilo kwa maslahi ya kisiasa.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)