Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtaka Rais Salva Kirr wa Sudan Kusini
na kiongozi wa waasi Riek Machar kufikia makubaliano kwa kwa shabaha ya
kuupatia ufumbuzi jumla mgogoro wa nchi hiyo changa zaidi barani
Afrika. Ban Ki-moon amesisitiza kwamba, pande mbili hasimu huko Sudan
Kusini zinapaswa kufikia makuabaliano na kuhitimisha mgogoro wa nchi
hiyo. Amesema hayo ikiwa kesho ndio siku ya mwisho ya muhula uliotolewa
na Jumuiya ya Kieneo ya IGAD kwa pande mbili hasimu huko Sudan Kusini
ziwe zimefikia makubaliano. Duru ya mwisho ya mazungumzo ya amani kwa
upatanishi wa Jumuiya ya Kieneo ya IGAD inatarajiwa kufikiwa kesho.
Licha ya juhudi kubwa za IGAD katika upatanishi wa mgogoro wa Sudan
Kusini, hadi sasa pande hizo hazijafikia makubaliano ya kuhitimisha
mgogoro huo. Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
limeunga mkono azimio la kuziwekea vikwazo pande mbili hasimu za Sudan
Kusini, endapo hazitafikia makubaliano katika muda ulioainishwa
unaomalizika kesho.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment