Siku kama ya leo miaka 1425
iliyopita, kwa mujibu wa baadhi ya nukuu za historia, Bibi Fatma Zahra
binti wa Mtume Muhammad SAW alikufa shahidi baada ya kuishi maisha
mafupi lakini yaliyojaa baraka tele. Baba yake ni Mtume Muhammad SAW na
mama yake ni Bibi Khadija binti Khuwaylid AS. Bibi Fatma alishiriki
katika medani mbalimbali za kipindi cha mwanzo wa Uislamu akiwa bega kwa
bega na Mtume wa Mwenyezi Mungu na Imam Ali bin Abi Talib AS na alilea
watoto wema, kama Imam Hassan na Hussein AS ambao Mtume (saw) amesema
kuwa ni viongozi wa mabarobaro wa peponi. Bibi Fatma alisifika mno kwa
tabia njema, uchaji Mungu na elimu, na alikuwa mfano na kiigizo chema
cha Waislamu.
Tarehe 4 Machi miaka 192
iliyopita, vikosi vya jeshi la Ugiriki vilifanya mauaji makubwa ya
halaiki dhidi ya Waislamu elfu 12 wakati wa vita vyao dhidi ya jeshi la
ufalme wa Othmania katika mji wa Tripolitsa. Makundi ya Wagiriki
waliokuwa wakiungwa mkono na nchi kadhaa za Ulaya, yaliungana na
kutekeleza mauaji hayo katika muongo wa mwanzoni mwa karne ya 19, yaani
mwaka 1822. Kufuatia mauaji hayo mwezi Novemba mwaka 1824 majeshi ya
utawala wa Kiothmani yaliamua kulipiza kisasi kwa kuua kundi la
Wagiriki.
Na siku kama ya leo miaka 167
iliyopita, yalianza mapambano ya wapigania uhuru wa Hungary dhidi ya
serikali ya Austria. Siasa za kibeberu za Klemens Metternich, Kansela wa
wakati huo wa Austria zilisababisha mapinduzi mwaka 1848 katika ardhi
zisizo za Ujerumani zilizokuwa chini ya himaya ya Austria, ikiwemo
Hungary. Uasi wa wananchi wa Hungary ulioibuka kutokana na dhulma ya
Waaustria, ulienea kwa kasi kote nchini humo. Licha ya kutishiwa na
serikali kuu, wanamapinduzi walitangaza nchi hiyo kuwa jamhuri tarehe 4
mwezi Aprili mwaka 1849 baada ya kushtadi harakati zao huko Hungary.
Hata hivyo kwa msaada wa utawala wa Tsar wa Urusi, ufalme wa Austria
uliyakandamiza mapinduzi hayo na kuwanyonga viongozi wake
0 comments:
Post a Comment