Mawaziri wa Utalii wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
wanatarajia kukutana mwishoni mwa mwezi huu kujadili pamoja na mambo
mengine, migogoro ya kimaslahi katika sekta ya utalii katika nchi zao.
Ajenda kubwa ya mkutano huo itahusu mgogoro kati ya Kenya na Tanzania
kuhusu kuzuiliwa kwa magari ya kusafirisha watalii kuingia na kutoka
katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Kupinga
Ujangili, Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Lazaro Nyalandu, amesema kuwa, wanatarajia kukutana Machi 20
jijini Arusha na kueleza kwamba, tofauti hizo zitajadiliwa na kupatiwa
ufumbuzi wa kudumu. Waziri Nyalandu amesema kuwa, Tanzania haitakubali
kupoteza maslahi ya Watanzania na taifa kwa ujumla. Amesema kama
ninavyomnukuu: "kilichotokea awali kwa sasa hakiko tena, mahusiano yetu
na Jamhuri ya Kenya ni mazuri, kwa sababu hiyo tumeafikiana na mawaziri
wa nchi hizo kukutana ili kuangalia njia ya kumaliza mvutano
unaoshindaniwa katika eneo hilo. Mwisho wa kunukuu. Ikumbukwe kuwa,
Desemba mwaka jana, serikali ya Kenya ilizuia magari yote ya Tanzania
yanayosafirisha watalii kutoka na kuingia katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta, hali ambayo imezua mikwaruzano kati ya Kenya
na Tanzania.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment