Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeendeleza operesheni zake
dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR kwa kushambulia ngome za waasi hao
mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya katikati mwa Afrika. Afisa mmoja wa
jeshi ambaye anashiriki kwenye operesheni hizo katika hifadhi ya taifa
ya Virunga, amesema kuwa, baada ya kutolewa amri ya kuwashambulia waasi
hao wa Kihutu, askari wa serikali walianzisha mashambulizi makali na
kufanikiwa kukomboa maeneo mengi kutoka kwa waasi hao. Mashirika kadhaa
yasiyo ya kiserikali mjini Kivu yamethibitisha habari hiyo. Kwa mujibu
wa habari, operesheni hizo zinafanyika katika eneo la Mabenga, Rutshuru
kwenye mpaka wa Kongo na nchi za Rwanda na Uganda. Mapigano makali ya
jana yalitokea katika milima ya maeneo hayo ambapo jeshi lilifanikiwa
kukomboa vijiji viwili kutoka mikononi mwa waasi hao wa Rwanda.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment