
Marekani inasema kuwa itafungua ubalozi wake nchini Cuba kuanzia mwezi Aprili.
Baada
ya duru ya pili ya mazungumzo mjini Washington yenye lengo la kurejesha
uhusiano kati yao mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Marekani katika
nchi za Marekani ya kusini Roberta Jacobson, alisema kuwa itawezekana
kufunguliwa kwa ubalozi kabla ya mkutano wa kimaeneo ambao utafanyika
nchini Panama kuanzia tarehe kumi mwezi Aprili.
Mkuu wa ujumbe wa
Cuba Josefina Vidal alisisitiza kuwa Marekani ni lazima iondoe Cuba
kutoka kwa orodha ya nchi ambazo zinaunga mkono Ugaidi kabla ya
kurejesha tena uhusiano huo.
Mwezi Disemba Cuba na Marekani walitangaza kuwa walikubaliana kuboresha uhusiano wao baada ya zaidi ya miaka 50 .
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment