Leo ni Jumatatu tarehe 26 Mfunguo Saba Rabiu Thani 1436 Hijria mwafaka na tarehe 16 Februari mwaka 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 23 iliyopita, inayosadifiana na
tarehe 16 Februari 1992 aliuawa shahidi katika shambulio la ndege za
utawala wa Kizayuni wa Israel Sayyid Abbas Musawi, Katibu Mkuu wa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon, huko
kusini mwa nchi hiyo. Shambulio hilo lilipelekea kuuawa pia watu kadhaa
waliokuwa wameandamana naye akiwemo mke na mwanawe mdogo, pamoja na
wasaidizi wake watatu. Shambulio hilo lilitokea wakati Sayyid Abbas
Musawi alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwenye kumbukumbu za kuuawa
shahidi Sheikh Raghib Harb aliyeuliwa na maafisa wa utawala huo miaka
michache iliyopita kabla ya hapo. Sheikh Raghib Harb alikuwa mwasisi wa
harakati za mapambano huko kusini mwa Lebanon. Hujuma hiyo ilizusha
hasira kubwa za Waislamu kote ulimwenguni dhidi ya Israel. Hata hivyo
madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu, si tu
hayakulaani jinai hiyo bali pia yalijaribu kuihalalisha. Baada ya kuuawa
shahidi Sayyid Abbas Musawi, Sayyid Hassan Nasrullah alichukua jukumu
la kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, na kutoa pigo kwa Israel mwaka 2000,
baada ya kuyafukuza kwa madhila majeshi ya utawala huo katika ardhi za
kusini mwa Lebanon.
Siku kama leo miaka 69 iliyopita, inayosadifiana na 16
Februari 1946 kwa mara ya kwanza kura ya veto ilitumiwa na mjumbe wa
Urusi ya Zamani katika Umoja wa Mataifa. Siku hiyo mwakilishi wa Urusi,
alipinga moja ya mapendekezo ya Baraza la Usalama na kutumia kwa mara ya
kwanza haki ya veto. Haki ya kura ya veto inayolalamikiwa na mataifa
mengine duniani zimepewa nchi tano tu wanachama wa kudumu katika Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa ambazo ni Marekani, Uingereza, Ufaransa,
China na Russia. Mpango wa kutumia veto ulipasishwa na Marekani,
Uingereza na Urusi ya Zamani katika mkutano wa Yalta wa mwaka 1945.
Tangu wakati huo kumekuwa na malalamiko ya kupinga kupewa nchi hizo tu
kura hiyo ya veto, hasa kwa kuzingatia kuwa, baadhi ya nchi hizo
zimekuwa zikiitumia haki hiyo kwa malengo ya kisiasa.
Na siku kama ya leo miaka 97 iliyopita, inayosadifiana na
tarehe 16 Februari 1918, Lithuania ilijitangazia uhuru wake baada ya
kudhoofika Russia kutokana na kushiriki kwake katika Vita Vikuu vya
Kwanza vya Dunia na kutokea mapinduzi nchini humo mwaka 1917. Pamoja na
hayo, Moscow iliendeleza mipango yake ya kuiunganisha tena Lithuania na
ardhi za Umoja wa Kisovieti, ambapo mwaka 1940 ilifanikiwa kufikia
lengo hilo. Ujerumani ya Kinazi iliikalia kwa mabavu Lithuania kwa zaidi
ya miaka mitatu katika kipindi cha Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia.
0 comments:
Post a Comment