Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
amekiri kwamba mshambuliaji wake nyota Alexi Sanchez huenda ameanza
kuonyesha ishara za uchovu.
Mchezaji huyo wa taifa la Chile
amefunga mabao 18 katika mechi 32 za the Gunners ,lakini Wenger anahisi
kwamba Sanchez hakucheza vyema wakati wa mechi ya ushindi dhidi ya
Leicester.Sanchez alipata jereha la mguu na hivyobasi kutolewa wakati wa mechi hiyo na sasa haijulikani iwapo atacheza mechi ya FA siku ya jumapili dhidi ya Middlesbrough.
''Hakucheza kama anavyocheza kila siku'',.alisema Wenger.
0 comments:
Post a Comment