Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa na
Kombe la Shirikisho, timu za Azam na Yanga zimeanza vema safari yao ya
kuwania makombe hayo baada ya kila timu kupata ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya wapinzani wao.
Ushindi huo unairahisishia Yanga kusonga mbele katika mchezo wa marudiano utakaofanyika mjini Gaborone wiki mbili zijazo.
Wachezaji wa timu ya Azam ya Tanzania
wakifurahia ushindi dhidi ya El-Merrekh ya Sudan kwa kuifunga 2-0 katika
mchezo uliofanyika Jumapili nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
Nao Azam, wawakilishi katika
kombe la klabu bingwa imeanza kampeni yake kwa kuinyuka El Merreikh ya
Sudan kwa magoli 2-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Azam Complex
Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam yalifungwa na Didier Kavumbagu na John Bocco.
Azam wa
natarajiwa kurudiana na El-Merreikh mjini Khartoum, wiki mbili zijazo.
Gor Mahia ya Kenya iliyoizamisha CNaps Sport ya
Madagascar bao 1-0 katika mchezo wao wa awali uliochezwa Jumamosi mjini
Nairobi
Matokeo ya timu nyingine za
ukanda wa Afrika Mashariki katika Kombe la Shirikisho la CAF, Polisi
Zanzibar imekumbana na kipigo kizito baada ya kuangushiwa mzigo wa mabao
5-0 dhidi ya CF Mounana ya Gabon na hivyo kujiweka katika mazingira
magumu ya kuendelea hatua ya pili.
Sofapaka ya Kenya nayo
imepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Platinum ya Zimbabwe kwa
kuchapwa magoli 2-1. Rayon Sport ya Rwanda imepata ushindi ugenini kwa
kuifunga Panthere ya Cameroon goli 1-0. Nayo URA ya Uganda imepata
ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Elgeco Plus ya Madagascar.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment