Serikali ya Siera Leone inasema kuwa
inatilia maanani ripoti maalum iliyogundua kuwa takriban dola milioni
14 zilizokuwa zitumike kupambana na ugonjwa wa ebola hazijulikani
zilipo.
Msemaji wa serikali (Abdulai Bayraytay) aliiambia BBC kuwa
yeyote ambaye atapatikana kuhusika kwenye ufisadi huo atakabiliwa na
mkono wa sheria.Mhasibu mkuu nchini humo ameshtumu wizara ya afya na idara inayohusika na ugonjwa wa ebola kwa kile alichokitaja kuwa ukiukaji wa sheria.
0 comments:
Post a Comment