Marekani imethibitisha kuwa
wanamgambo wa Islamic State wameuteka mji wa Ali Baghdadi ulio mashariki
mwa Iraq karibu na kituo cha jeshi la Marekani.
Msemaji wa makao
makuu ya jeshi la Marekani (John Kirby) alisema kuwa ni mara ya kwanza
kwa miezi kadhaa ambapo wanamgambo wa islamic state wameliteka eneo
jipya.Mji wa Al Baghadad ulio kwenye mkoa wa Anbar uko umbali wa chini ya kilomita 10 kutoka kituo cha jeshi la wanahewa 300 wa Marekani wanaowapa mafunzo wanajeshi wa Iraq.
Mapema wanajeshi wa Iraq walikabiliana na kile kilichoonekana kuwa shambulizi la kujitolea muhanga dhidi ya kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment