Kamanda wa polisi kaunti ya Homa Bay John Omusanga amesema, watoto wawili wamefariki kwenye ajali hiyo iliyotokea saa nane usiku karibu na kisiwa cha Remba. Watoto hao wametambuliwa kwa majina ya Fatou Bensouda, aliyekuwa na umri wa miaka 2, na Eda Anyango alioyekuwa na umri wa miaka 4. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Nyanza Willy Lugusa amesema, wengi wa watu walionusurika waliokolewa na wavuvi. Amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linaongoza operesheni ya uokoaji, na idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa kuwa watu wengi bado hawajulikani walipo.
0 comments:
Post a Comment